MSTAHIKI
Meyawa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameandaa mashindano ya mashairi
yatakayofanyika Julai 30 na 31, Mwaka huu katika viwanja vya Karemjee jijini.
Akizungumza na Fichua, Mwita alisema lengo la mashindano hayo ni kukumbuka
historia ya jiji la Dar es Salaam ambalo lilisifika kwa ushairi na tenzi nzuri.
Alisema
mashairi hayo yataghaniwa na wazee wa jiji la Dar es Salaam ambao watawakilisha
mada mbalimbali katika utunzi wao.
“Tungependa
watukumbushe historia ya Mzizima ilikuwaje, Mwalimu Julias Nyerere alipoingia
Dar es Salaam walimpokeaje na kwa nini maadili ya vijana yanamomonyoka,”
alisema Mwita.
Alisema
watakaa kila mwaka mara mbili kuikumbuka historia ya jiji la Dar es Salaam.
Aidha
alisema Septemba 23 na 24, mwaka huu kutakuwa na maonyesho ya utalii wa ndani
ambapo ngoma kutoka katika makabila mbalimbali ya Tanzania.