Monday, July 6, 2015

TTCL KUPELEKA MAWASILIANO KWA WATEJA WALIO NJE YA MKONGO



KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL), imeanza kuwawezesha wateja wake yakiwamo makampuni, taasisi na ofisi za Serikali kupata mawasiliano ya intaneti sehemu zilizo mbali na njia ya mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.

Taarifa hiyo ilitolewa na Ofisa Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi wa TTCL, Fredrick Bernad alipokuwa akizungumza katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam maarufu kama maonyesho ya Sabasaba.
Kwa mujibu wa Benard, teknolojia hiyo ni mpya na ni muhimu kwa kampuni na wateja wengine kwani ni bora na ni ya uhakika kwa mawasiliano.
“Mbali na mawasiliano ya intaneti, wateja wanaweza pia kupata huduma ya kupata mawasiliano ya shughuli za kiofisi zaidi ya mbili ambazo zipo maeneo tofauti na kushirikiana kwa taarifa na mifumo ya kompyuta iitwayo Mpls Vpn.

“TTCL iliamua kuleta huduma hiyo kutokana na mahitaji makubwa ya matumizi ya intaneti kwa shughuli za maendeleo kwani kuna maeneo ambayo awali yalihitaji huduma ya mkongo lakini kutokana na umbali pamoja na gharama imekuwa ngumu kuwapelekea huduma.

ORODHA YA VYUO FEKI INDIA



WATANZANIA wengi wanapenda kusoma vyuo vikuu nje ya nchi kutokana na kudhani  kuwa nje ya nchi ndipo inapopatikana elimu bora na ya  uhakika.
Wengi wao husoma nje ya nchi bila kuchunguza kama hivyo vyuo vimesajiliwa  na serikali ya nchi hiyo au laa, hali inayopelekea kujikuta wakisoma katika vyuo visivyo na vigezo.
Hivi karibuni,baraza la taifa la elimu ya  ufundi( NECTA) limetoa idadi ya  vyuo ambavyo havijasajiliwa  na vingine kuwa chini ya viwango    
ORODHA YA VYUO BANDIA HUKO INDIA KAMA ILIVYOTOLEWA LEO
Here is the list of the fake universities:
1. Maithili University, Darbhanga, Bihar
2. Varanseya Sanskrit Vishwavidyalaya, Delhi
3. Commercial University Ltd, Delhi
4. United Nations University, Delhi
5. Vocational University, Delhi
6. ADR- Central Juridical University, Delhi
7. Indian Institution of Science and Engineering, Delhi
8. Badagnavi Sarkar World Open Educational Society, Belgaum, Karnataka
9. St. John's University, Kishanattam, Kerala
10. Kesarwani Vidyapith, Jabalpur, Madhya Pradesh
11. Raja Arabic University, Nagpur, Maharashtra
12. D D B Sanskrit University, Putur, Trichy, Tamil Nadu
13. Indian institute of Alternative Medicine, Kolkata, West Bengal
14. Mahila Gram Vidyapith, Allahabad, Uttar Pradesh
15. Gandhi Hindi Vidyapith, Allahabad, Uttar Pradesh
16. National University of Electro Complex Homeopathy, Kanpur, Uttar Pradesh
17. Netaki Subhash Chandra Bose University, Aligarh, Uttar Pradesh
18. Uttar Pradesh Vishwavidyalaya, Uttar Pradesh
19. Maharana Pratap Shiksha Niketan Vidyalaya, Pratapgarh, Uttar Pradesh
20. Indraprastha Shiksha Parishad, Noida-Phase II, Uttar Pradesh
21. Gurukul Vishwavidyalaya, Mathura, Uttar Pradesh.