KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL), imeanza
kuwawezesha wateja wake yakiwamo makampuni, taasisi na ofisi za Serikali kupata
mawasiliano ya intaneti sehemu zilizo mbali na njia ya mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano.
Taarifa hiyo ilitolewa na Ofisa Mtatuzi wa
Masuala ya Kiufundi wa TTCL, Fredrick Bernad alipokuwa akizungumza katika
Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar
es Salaam maarufu kama maonyesho ya Sabasaba.
Kwa mujibu wa Benard, teknolojia hiyo ni mpya
na ni muhimu kwa kampuni na wateja wengine kwani ni bora na ni ya uhakika kwa
mawasiliano.
“Mbali na mawasiliano ya intaneti, wateja
wanaweza pia kupata huduma ya kupata mawasiliano ya shughuli za kiofisi zaidi
ya mbili ambazo zipo maeneo tofauti na kushirikiana kwa taarifa na mifumo ya
kompyuta iitwayo Mpls Vpn.
“TTCL iliamua kuleta huduma
hiyo kutokana na mahitaji makubwa ya matumizi ya intaneti kwa shughuli za
maendeleo kwani kuna maeneo ambayo awali yalihitaji huduma ya mkongo lakini
kutokana na umbali pamoja na gharama imekuwa ngumu kuwapelekea huduma.
No comments:
Post a Comment