Friday, July 22, 2016

Mashindano ya mashairi kufanyika Julai 30



MSTAHIKI Meyawa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameandaa mashindano ya mashairi yatakayofanyika Julai 30 na 31, Mwaka huu katika viwanja vya Karemjee jijini. 
Akizungumza na Fichua, Mwita alisema lengo la mashindano hayo ni kukumbuka historia ya jiji la Dar es Salaam ambalo lilisifika kwa ushairi na tenzi nzuri.
Alisema mashairi hayo yataghaniwa na wazee wa jiji la Dar es Salaam ambao watawakilisha mada mbalimbali katika utunzi wao.
“Tungependa watukumbushe historia ya Mzizima ilikuwaje, Mwalimu Julias Nyerere alipoingia Dar es Salaam walimpokeaje na kwa nini maadili ya vijana yanamomonyoka,” alisema Mwita.
Alisema watakaa kila mwaka mara mbili kuikumbuka historia ya jiji la Dar es Salaam.
Aidha alisema Septemba 23 na 24, mwaka huu kutakuwa na maonyesho ya utalii wa ndani ambapo ngoma kutoka katika makabila mbalimbali ya Tanzania.

mchekeshaji mwingine afariki dunia



Msanii wa Vichekesho Ismail Makombe maarufu Baba Kundambanda afariki dunia asubuhi ya leo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu zinasema Kundambanda amefariki alfajiri ya leo mjini Masasi kutokana na maradhi ya kifua.
“Juzi alibanwa na kifua akaenda mwenyewe hospitali huku akiendesha gari, akapatiwa matibabu na jana kuanzia mchana ndipo hali ilipobadilika na hatimaye leo alfajiri kufariki dunia,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilisema kuwa taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwake Masasi
FICHUA inawatakia subira wafiwa wote na mungu aipumzishe roho ya marehemu pema peponi. amen
 

SIKU YA FAMILIA YA MSONDO JUMAPILI



BENDI ya Msondo Ngoma imewataka mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi nchini kujitokeza katika tamasha la siku ya Familia litakalofanyika leo katika ukumbi wa DDC Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Meneja wa bendi hiyo, Said Kibiriti aliliambia DIMBA kuwa lengo ni kuwa na wasaa wa kukutana na mashabiki wao ikiwa ni pamoja na kubadilishana mawazo na kuichangia bendi hiyo ili iweze kufanya vema.
Alisema onesho hilo litawakumbusha mashabiki kuwa bendi ipo na inaendelea kufanyakazi vizuri.
“Katika onesho hilo tunatarajia kutambulisha nyimbo mpya mbili ambazo ni ‘Masimango’ ukiwa ni utunzi wa Edo Sanga na ‘maana ya ndoa iko wapi’ ukiotungwa na mwanamuziki Athumani Kambi,” alisema Kibiriti.
mwisho