Friday, July 22, 2016

Mashindano ya mashairi kufanyika Julai 30



MSTAHIKI Meyawa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameandaa mashindano ya mashairi yatakayofanyika Julai 30 na 31, Mwaka huu katika viwanja vya Karemjee jijini. 
Akizungumza na Fichua, Mwita alisema lengo la mashindano hayo ni kukumbuka historia ya jiji la Dar es Salaam ambalo lilisifika kwa ushairi na tenzi nzuri.
Alisema mashairi hayo yataghaniwa na wazee wa jiji la Dar es Salaam ambao watawakilisha mada mbalimbali katika utunzi wao.
“Tungependa watukumbushe historia ya Mzizima ilikuwaje, Mwalimu Julias Nyerere alipoingia Dar es Salaam walimpokeaje na kwa nini maadili ya vijana yanamomonyoka,” alisema Mwita.
Alisema watakaa kila mwaka mara mbili kuikumbuka historia ya jiji la Dar es Salaam.
Aidha alisema Septemba 23 na 24, mwaka huu kutakuwa na maonyesho ya utalii wa ndani ambapo ngoma kutoka katika makabila mbalimbali ya Tanzania.

No comments:

Post a Comment