UONGOZI wa Serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es
Salaam(DARUSO), umeiomba serikali kuacha urasimu wa kuwalipa fedha za mikopo na
badala yake watekeleze kama walivyokubaliana katika mikataba yao.
Akizungumza jana wakati wakifanya mgomo baridi kushinikiza
kulipwa fedha zao za kujikimu,Waziri wa Mikopo ya wanafunzi wa chuo hicho,
Shitindi Venance alisema inashangaza kuona baadhi ya viongozi wa serikali ambao
wamekuwa wakitumia mabilioni ya fedha wakidai ni ya mboga wakati wao
wakishindwa kutekelezewa ahadi za mikataba yao.
“Nchi hii imefikia pabaya, inashangaza Waziri anayekumbwa
na kashfa anatangaza kuwa bilioni 10 ni fedha za mboga wakati sisi tunadai
bilioni 2.8 za kujikimu kwa wanafunzi 6120 wameshindwa kutulipa jambo ambalo
linatujengea taswira mbaya,” alisema Venance.
Venance alisema serikali iache kufanya kazi kwa mazoea kwa
kusubiri shinikizo la migomo ndipo watekeleze majukumu yao kwani wanajijengea
muundo mbaya.
Alisema viongozi wengi walioko madarakani wanatumia vibaya
nyazifa na fedha zao kuwalaghai wanafunzi wa kike nao kwa shida walizonazo
wanakubali kuingia kwenye mitego yao.
“Wasifikiri hatuoni wanavyokuja na mashangingi kuwalaghai
dada zetu wakati hawataki kuwapi fedha zao kwa wakati wawalipe ili wasiingie
vashawishini,” alisema venance.
Alisema waliingia mkataba na Bodi ya Mikopo kuwa kila baada
ya wiki nane watakuwa wanawaingizia 450,000 fedha za kujikimu lakini hadi sasa
wiki ya 11kiongozi yeyote aliyelizungumzia hilo.
Aliongeza kuwa baada
ya kuona kuwa fedha hazijaingizwa walienda hadi Bodi ya Mikopo ambao nao
walidai hawajapewa fungu hilo na walipoenda Wizara ya Fedha bado hakukuwa na
jibu la kueleweka.
“Tunaupongeza uongozi wa Chuo ambao umeahidi kutukopesha
shilingi 20,000 ili kupunguza makali japokuwa fedha hizo hatukuzipokea kwa kuwa
hazitosherezi mahitaji yetu,” alisema.
Alisema wamekuwa
wakisoma kwa shida kwa muda mrefu ambapo
hata mwaka jana walienda kufanya mafunzo kwa vitendo(field
attachment)bila kulipwa fedha hadi waliporejea.
“Mwaka huu tunatangaza kabisa kama fedha za ‘field’ hakuna
hatuendi,” alisema.
Alisema Serikali inawafundisha vibaya kuwa bila kuiadhibu
haitekelezi jambo.
“Baada ya leo (jana) kuanza kushinikiza mgomo kwa kukataa
kuingia darasani, tumeambiwa lazima ziingie… nasi hatulali leo kama fedha
hazijaingia tutakesha,” alisema.
BLOG hii ilifika chuoni hapo na kuwakuta wanachuo wakiwa
wamekusanyika eneo moja huku wakiwa wametulia wakisubiri maagizo ya viongozi ambao
walikuwa wakihaha huku na kule kujua hatma yao bila ya kuleta taharuki ndani ya
chuo.
Kwa upande wake Msemaji wa Bodi ya mikopo ya Wanafunzi,
Cosmas Mwaisobwa alisema madai ya wanafunzi hao yanashughulikiwa na si chuo
hicho tu.
“Ni kweli baadhi ya
wanafunzi wanadai na madai yao yanashughulikiwa na si chuo hicho tu kuna vyuo
vingi ambavyo vina madai kama hayo
No comments:
Post a Comment