WIZARA ya Afya na
Ustawi wa Jamii imetuma wataalamu katika mkoa wa Simiyu ambako kumeripotiwa
kuwepo na ugonjwa unaosababisha watu kuongea ovyo.
Ugonjwa huo uliibuka mwanzoni
mwa mwezi huu wilayani Meatu mkoani Simiyu na kusababisha watu 80 kuugua.
Akizungumza jana, Msemaji wa wizara hiyo, Nsachris Mwamwaja, alisema wataalamu
hao walitumwa wiki iliyoita na wanaendelea na uchunguzi ili kubaini ni aina
gani ya ugonjwa.
“Tayari kuna sampuli
zimeletwa Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi...unaweza ukawa unaongea ovyo
lakini wakachukua sampuli za damu hivyo tusubiri majibu,” alisema Mwamwaja.
Alisema uchunguzi wa
awali umebaini kuwa watu hao pia walikuwa na magonjwa mengine ya kuhara na
kutapika.
Baadhi ya waathirika
waliofikishwa katika vituo vya afya walipimwa na kubainika hawana ugonjwa
wowote na badala yake kubaki wakiweweseka.
Mkuu wa wilaya ya
Meatu, Erasto Sima alisema kuwa ugonjwa huo ulizikumba kata za Mwandoya,
Mwabusalu, Lingeka, Mwakisandu, Tindabuligi na Lubiga.
Kulingana na Mkuu
huyo wa Wilaya, baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakiishiwa nguvu, kuongea maneno
yasiyoeleweka, kuwapiga wenzao, kugongwa na kichwa, kutokwa na mafua na kukohoa
kikohozi kikavu.
No comments:
Post a Comment